judo

JATA wapata ofisi Dar

RAIS wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Khalifa Kiumbe ‘Chief Kiumbe’, ameanza kazi kwa makeke baada ya kupata ofisi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Chief Kiumbe alisema kuwa lengo lake ni kufanya mchezo huo kuwa wa kimataifa zaidi na si kuwa na ofisi mkononi kama ilivyokuwa awali.

“Ili chama kiweze kuheshimiwa ni lazima kiwe na ofisi inayoeleweka ambapo hata waandishi watakuwa huru kututembelea na kupata maendeleo ya mchezo huo,” alisema Chief Kiumbe.

Rais huyo ambaye ameingia madarakani hivi karibuni, alisema kuwa ataitambulisha rasmi ofisi hiyo baada ya kukamilisha mambo ambayo sio vema kuyataja kwa sasa.

JATA chini ya Katibu, Shabani Kashinde, haikuwahi kuwa na ofisi, kitu ambacho kilikuwa kikisababisha usumbufu wa kupata taarifa, huku hata mihuri ya chama ilikuwa ikihifadhiwa kwa katibu huyo ambaye amefungiwa kujihusisha na michezo maisha, baada ya kutuhumiwa kusafirisha watu ambao si wanamichezo nje ya nchi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.