gofu

Tanzania yaanza vibaya gofu Afrika Kusini

Mbonile Burton

WACHEZAJI wa Tanzania wameanza vibaya kwenye michuano ya gofu ya wanawake ya Sanlam Afrika Kusini (Sanlam Women’s Amateur SA Stroke Play Championship) iliyoanza juzi kwenye Viwanja vya Klabu ya Umhlali Country, KwaZulu Natal.

Katika michuano hiyo wachezaji wawili wa Tanzania akiwepo nahodha wa timu ya Taifa Madina Iddi na Angel Eaton ni miongoni mwa zaidi ya wachezaji 120 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaoshiriki.

Katika raundi hiyo ya kwanza nahodha Madina alirejea na mikwaju 86, katika nafasi ya 73, wakati Eaton alipiga mikwaju 81 nafasi ya 40 hivyo, kujiweka kwenye wakati mgumu katika mbio za ubingwa.

Madina anayechezea handicap 3 ambaye alifika Afrika Kusini siku moja kabla ya michuano kuanza alifanya kazi ya ziada kurejea na mikwaju hiyo kutokana na kuhaha kuendana na hali ya hewa ya huko ambayo ilikuwa na upepo mkali, wakati Angel (handicap 1) yupo Afrika Kusini kwa miezi kadhaa sasa.

Hali hiyo inawafanya kuwa na kibarua kigumu katika raundi mbili zilizosalia ikiwepo jana na leo katika michuano hiyo ya viwanja 54.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.