VPL

Aggrey mchezaji bora, Hall kocha bora VPL 2011/12


Nahodha wa Azam FC Aggrey Morice amefanikiwa kutwa tuzo ya tatu katika mwaka huu wa 2012, baada ya jana usiku kutangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya vodacom msimu wa 2011/12.

Aggrey alianza kupokea tuzo ya mchezaji muhamasishaji wa klabu ya Azam FC zilizotolewa mara baada ya msimu kumalizika, ikifuatiwa tuzo ya mwanasoka bora wa Tanzania katika msimu wa 2011/12 zilizotolewa na chama cha waandishi wa habari za michezo 'TASWA'.

Katika utoaji wa Tuzo hizo hapo jana katika hotel ya Double tree By Hilton, kipa wa Simba SC Juma Kasija alitwaa tuzo ya kipa bora huku, kiungo Frank Domayo aliyejiunga Yanga akitokea JKT Ruvu, Rashid Mandawa wa Coastal union pamoja Hassan Dilunga wa Ruvu shooting wamejizolea mili 1 kila mmoja, baada ya kuibuka chipukizi bora toka katika vikosi B kupandishwa vikosi A vya timu zao.

Mabingwa wa Mapinduzi walijizolea tuzo ya timu yenyenidhamu, japo kuwa michezo iliyohusisha timu hiyo kuwa na vurugu. Michezo hiyo ni ule dhidi ya Yanga, Polisi Dodoma na Mtibwa Sugar.

Mshambuliaji wa Azam FC John Bocco alitwa tuzo ya Mfungaji bora, wakati kocha wake Stewart Hall akichukua tuzo ya kocha bora.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.