VPL

MBEYA CITY WAENDELEZA UBABE KWA PRISONS, COASTAL WAKILALA

Mbeya city hii leo wameendeleza wimbi la ushindi na kufanikiwa kupunguza tofauti ya pointi baina yake na Yanga waliyo nafasi ya pili wakati Mbeya city ikiwa nafasi ya 3.

Mbeya city hii leo walikuwa katika uwanja wa Sokoine kuwakabili jirani zao wa Tanzania Prisons mchezo uliomalizika kwa Mbeya city kuwachapa goli 1-0.

Goli la Mbeya city lilifungwa na Paul Nonga katika dakika ya 46 na kuipelekea kumaliza mchezo na mshindi wa goli 1-0.


Katika uwanja wa Manungu, Morogoro Mtibwa sugar waliwalaza Coastal union goli 3-1.

Magoli ya washindi Mtibwa sugar yalifungwa na Jamali Mnyate katika dakika ya 14, Mussa Hassan Mgosi katika dakika ya 31 na Mkopi katika kipindi cha pili, wakati goli la Coastal union likifungwa na Mbwana katika dakika ya 17.



MATOKEO MENGINE YA LEO:

JKT RUVU 3-1 RHINO RANGERS
KAGERA SUGAR 0-0 RUVU SHOOTING

AZAM FC 2-1 SIMBA SC
MGAMBO SHOOTING 2-1 YANGA
MTIBWA SUGAR 3-1 COASTAL UNION
MBEYA CITY 1-0 T.PRISONS

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.