VPL

AZAM WABANWA, COASTAL WAKITAMBA

picha kwa msaada wa kurasa wa Coastal Uniom; COASTAL 2-0
Makamu bingwa wa ligi kuu ya vodacom Azam FC wameanza vibaya msimu mpya wa ligi kuu ya vodacom baada yak uwambulia sare ya goli 1-1 toka kwa wakatamiwa wa Turiani Mtibwa sugar mchezo uliochezwa katika uwanja wa Manungu Complex.

Katika mchezo huo ambao Mtibwa sugar waliutawala na kuipa kazi ya ziada ngome ya Azam FC walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 6 kupitia kwa mshambuliaji wao chipukizi Juma Lizao akiunga vyema pande la kiungo mchezeshaji wazamani wa SC Villa na Simba SC Shabani Kisiga.

Goli hilo liliendelea kuwapa nguvu Mtibwa sugar ya kulishambulia lango la Azam FC lakini jitihada ya mlinda mlango kinda Aishi Manula pamoja na safu yake ya ulinzi iliweza kuondosha hatari hizo.

Azam FC walisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati uliopigwa na beki Aggrey Morice na kupelekea mchezo kwenda mapumziko milango ikisomeka 1-1.

Azam FC walianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ambapo aliingi Kipre Bolue katika nafaci ya Himid Mao na Khamisi Mcha katika nafasi ya Ibrahim Mwaipopo mabadiliko ambayo yalipelekea timu hizo kushambuliani kwa zamu.

Katika dakika mbili za nyongeza kama Azam FC wangekuwa makini wangeweza kupata goli la ushindi baada ya kulisaka lango la Mtibwa Sugar kwa dakika zote mbili ikiwa Mtibwa Sugar wakitokea kupoteza nafasi kupitia kwa Mussa Mgosi, na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Vodacom uliwakutanisha mabingwa wazamani wa Tanzania BAra Coastal union na wenyeji wao JKT Oljoro na mchezo kumalizika kwa Coastal Union kuibuka na point zote tatu kwa kuifunga goli 2-0 wanajeshi hao wa kujenga kambi.

Magoli ya Coastal union yalipatikana kupitia kwa Abdi Banda katika dakika ya 18 kabla ya Criford Udula kuwainuwa Wagosi wakaya Coastal union kwa kuipatia goli la 2 na la mwisho kwa siku ya leo kwa Coastal Union.

 

MATOKEO MENGINE YA VPL

MGAMBO SHOOTING 0-2 JKT RUVU
RUVU SHOOTING 3-0 TANZANIA PRINSONS
MBEYA CITY 0-0 KAGERA SUGAR
SIMBA SC 2-2 RHINO RANGER
YANGA 5-1 ASHANTI UNITED
MTIBWA SUGAR 1-1 AZAM FC
JKT OLJORO 0-2 COASTAL UNION

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.