gofu

KAIN MBAYA, WAITARA WATESA

Kain Mbaya wa klabu ya Lugalo aliibuka mshindi wa jumla kwa kupiga mikwaju ya netti 143 katika mashindano ya NIC Captain Challenge troph  yaliyofanyika kwenye viwanja vya Lugalo mwishoni mwa wiki.

Mashindano hayo ya gofu yalifanyika kwa siku mbili  yalishirikisha wachezaji zaidi ya 80 kutoka klabu za Dar es Salaam Gymkhana, Morogoro na Lugalo yenyewe.
Kain siku ya kwanza alipata netti 71, na siku ya pili akapata netti 72, naye Abdalah Yusuph wa klabu ya  Lugalo alipata ushindi wa jumla kwa gross 151.
Kwa upande wa daraja A mshindi alikuwa Athumani Chiundu aliyeshinda kwa netti 146, nafasi ya pili ikaenda kwa Iddi Mzaki aliyepata netti 153.
Upande wa daraja B mshindi alikuwa Sodison Manasa aliyeshinda kwa mikwaju ya netti 145, huku Samweli Hagu akishika nafasi ya pili baada ya kushindwa kwa ‘Countback’.
Naye Patrick Waweru alishinda kwa upande wa daraja C kwa mikwaju ya nett 151, nafasi  ikaenda kwa Nichorausi Chitanda aliyepata netti 170.
Upande wa ‘Senior’ mshindi alikuwa Jeneral George Waitara aliyeshinda kwa netti 152 na kufuatiwa naJob Masima aliyepata netti 152.


CHANZO: MWANANCHI

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.