CECAFA

ATUDO AZIKUTANISHA KENYA NA KILI STARS NUSU FAINALI


 http://static.goal.com/245400/245448_heroa.jpg

Beki wa limataifa wa Azam FC toka nchini Kenya Joackins Atudo ameiwezesha timu yake ya Taifa kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watacheza dhidi ya Tanzania Bara siku ya jumanne ikiwa ni nusu fainali ya kwanza ya kombe la Chalenge linalo endelea nchini Kenya.

Atudo hii leo ameifungia Kenya goli pekee la ushindi kwa mkwaju wa penati uliopigwa katika ya 56 na kuipa ushindi Kenya wa goli 1-0 mbele ya Rwanda.

Tanzania Bara ambao nao wametinga katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuwalaza mabingwa watetezi kwa mikwaju ya penati 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya goli 2-2.

 Sasa nusu fainali ya kwanza itawakutanisha Kenya na Tanzania bara siku ya jumannem, wakati ya pili itawakutanisha washindi wa michezo ya kesho ya robo fainali ambapo Ethiopia watakutana na Sudan na  mchezo mwingine ni kati ya Zambia na Burundi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.