zanzibar

BLACKSAILOR, UJAMAA WATINGA ROBO KOMBE LA MTAONO

TIMU ya Soka ya Blacksailor na Timu ya Ujamaa zimefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Mtoano baada ya kushinda katika michezo yao waliocheza juzi.

Black Sailor ambayo ilishuka katika Uwanja wa Mao Tse Tung saa 8:00 mchana iliifunga Mwembeladu mabao 3-1 wakati Ujamaa iliifunga West Coast bao 1-0 ambayo ilicheza uwanjani hapo saa 10:00 za jioni.

Michezo yote hiyo ilikuwa na ushindani kiasi huku Blacksailor ikijipatia ushindi huo kupitia kwa wachezaji wake Yunnus Abaddal dakika 36, Abdul Ameir dakika 40 na Khamis Maulid dakika 55, huku bao la wapinzani wao likifungwa na Sleyoum Abdalla dakika 66.

Kwa upande wa timu ya Ujamaa iliweza kujipatia ushindi huo kwa bao la pekee lililofungwa na Hassan Bakari katika dakika ya 76.

Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo uwanjani hapo kwa michezo miwili ya kumalizia hatua ya awali ambapo mchezo wa kwanza utachezwa saa 8:00 mchana kati ya Vikokotoni na Polisi na wa pili utachezwa saa 10:30 kati ya Kilimani City na Shangani FC.


CHANZO: HABARI LEO

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.