CECAFA

KILI MANJARO STARS WAPIGWA NA KENYA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwCblDiT0JkZqZemzmoHBg_Y0SHBsJRn51cW3LL2frDlv2keB6EoCytn67EH7uhUqPoKNHF_jKDm6KYYUa2d4EHvDzkZC7FVsNhxdxcGO-F-8N_HdR8k9vXZKnC63qcQ6AXdG0bY2Qpcc/s1600/3.jpg

Kwa mara nbyingine tena timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro stars' imeshindwa kutnga hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA Chalenge cup baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 mbele ya wenyeji wa michuano ya mwaka huu Kenya 'Harambe stars'.

Mchezo huo wa nusu fainali ulipaswa kuchezwa saa nane mchana mjini Machakos Kenya lakini kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha katika eneo hilo ulipelekea mchezo kuamishiwa katika uweanja wa Nyayo mjini Nairobi baada ya uwanja wa Machakos kujaa maji.

Katika mchezo huo ulianza saa moja usiku Kenya waliandika goli lao la kuongoza katika dakika ya 4 kupitia kwa mshambuliaji wa Thika United, Clifton Miheso kwa shuti la umbali wa mita 20, baada ya kupokea pasi fupi ya Alan Wanga na kumchungulia kipa Ivo Mapunda.

Kwa matokeo hayo, sasa Stars itamenyana na Zambia katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu keshokutwa mchana Uwanja wa Nyayo tena, wakati Kenya itamenyana na Sudan katika Fainali jioni yake.

Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Michael Pius, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk65, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba/Farid Mussa dk65.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.