MAAFANDE wa KMKM wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya soka ya kombe la Mtoano kwa kuwafunga Shangani bao 1-0, katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mao Tse Tung juzi.
Katika mchezo huo, maafande hao walisumbuliwa na ngome ya wapinzani wao ambao waliwalazimisha kwenda mapumziko wakiwa hawajafungana.
KMKM baada ya kuona hali inakuwa sio nzuri ilifanya mabadiliko ya washambuliaji wake kwa kumtoa Ali Ahmed Shiboli na kumuingiza Ame Khamis Kibobea mabadiliko ambayo yalionekana kuzaa matunda.
Bao hilo pekee ambalo ndilo lililowaondosha uwanjani hapo kifua mbele lilifungwa na mchezaji wake Haji Simba baada ya kuwatoka walinzi wa Shangani na kuingiza mpira huo moja kwa moja wavuni.
Mbali na mchezo huo, juzi pia ulichezwa mchezo kati ya Kijangwani na SICCO ambapo SICCO ilishinda kwa mikwaju ya penanti 4-1 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 wakiwa sare ya kufungana bao 1-1.
CHANZO: HABAR LEO

0 comments:
Post a Comment