Magoli mawili ya Hamisi Tabwe na moja la Awadhi Juma yalitosha kuwapa ushindi wa goli 3-1 Simba SC mbele ya mtani wake Yanga SC katika mchezo wa hisani wa mtani jembe uliochezwa katika uwanja wa Taifa hii leo,
Katika mchezo huo Simba SC walianza kuandika goli la kwanza katika dakika ya 10 kupiti kwa Hamisi Tabwe.
Katika mchezo huo Simba SC walianza kuandika goli la kwanza katika dakika ya 10 kupiti kwa Hamisi Tabwe.
![]() |
| Hamisi Tabwe akifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati |
Simba walirejea tena katika nyavu za yanga katika dakika ya 41 kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Haisi Tabwe baada ya Ramadhan Singano Kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari, na penati hiyo kuzaa goli la pili.
Katika kipindi cha pili Simba waluanza kwa kurejea nyuma huku Yanga wakiwa wanasaka golikwa udi na uvumba.
Katika kipindi cha pili Simba waluanza kwa kurejea nyuma huku Yanga wakiwa wanasaka golikwa udi na uvumba.
Alikuwa Awadhi JUma aliyetokea benchi akifunga goli la tatu kwa Simba SC katika dakika ya 62 na kurejesha utawala wa mchezo kwa simba SC.
Katika mchezo huo ulioshuhudia mabadiliko mengi ya wachezaji beki Kelvin Yondani alizawadiwa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo Ramadhan Singano na kuzawadiwa kadi ya pili ya njano na kuonyeshwa kadi nyekundu.
Goli pekee la Yanga lilifungwa na Emanuel Okwi aliyetokea benchi akiunga krosi ya Saimon Msuva katika dakika ya 80.

0 comments:
Post a Comment