TIMU ya soka ya wasichana chini ya umri wa miaka 20 ‘Tanzanite’ jana iliaga michuano ya kimataifa baada ya kufungwa mabao 5-0 na wenzao wa Afrika Kusini.
Tanzanite ilikuwa ikishiriki michuano ya awali kuwania kufuzu kombe la dunia kwa wasichana wa umri huo, na hiyo ilikuwa mechi ya raundi ya pili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Soweto kwenye uwanja wa Dobsonville ilipochezwa mechi hiyo, wenyeji walitawala kila idara na kuifanya Tanzanite kushindwa kufurukuta.
Matokeo hayo yanaifanya Tanzanite iondolewe kwa jumla ya mabao 9-1 baada ya kufungwa mabao 4-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Akizungumza kutoka Soweto, kocha wa Tanzanite, Rogasian Kaijage, alisema matokeo yasiwakatishe tamaa watanzania kwani wachezaji wake wamejaribu.
“Tumefungwa, lakini haimaanishi kwamba watu wakate tamaa, hapana wachezaji wamejaribu na ikumbukwe kuwa timu hii ndio inajengwa,” alisema Kaijage.
“Wenzetu wana uzoefu nasi ndio tunaanza, hatukuwa na timu ya vijana upande wa wanawake, hivyo ndio tunaanza kujenga timu, tutakuwa vizuri tu,” alisema Kaijage.
Tanzanite ilifuzu kucheza raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondoa mashindanoni Msumbiji kwa jumla ya mabao 15-1, ikishinda mabao 10-0 nyumbani na kushinda mabao 5-1 Msumbiji.
Afrika Kusini sasa itacheza na mshindi wa mechi kati ya Nigeria na Burkina Faso kabla ya kufuzu michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Canada mwakani.

0 comments:
Post a Comment