SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeishukuru Serikali kuwaombea Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuwapa nafasi ya kuandaa mashindano ya Kombe la Afrika la Vijana. TFF inatarajia kuwa mwenyeji michuano ya vijana mwaka 2019, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepeleka maombi CAF ikitaka kuwapa ushirikiano TFF endapo itakubali ombi hilo.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema Serikali imeonesha imani kubwa kwa shirikisho hilo. Aliishukuru Serikali hasa Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kwa kuwaunga mkono kuandaa michuano hiyo.
Alisema Serikali imefanya kitu cha kiungwana na kuongeza kuwa kwa ushirikiano huo inaashiria kuwa hata ombi la kuandaa mashindano hayo litakubaliwa na hatimaye kufanyika kama ilivyopangwa.
“Binafsi kwa niaba ya TFF na wapenzi wa mpira kwa ujumla, tunaishukuru Serikali hasa Rais Kikwete na Waziri wa Michezo Dk Fenella kwa kuiandikia CAF barua na kuitaka kutupa ushirikiano katika suala hili," alisema Malinzi aliyeingia madarakani Oktoba 27, mwaka huu.
Kwa upande mwingine, Malinzi alisema wamewasilisha ombi CAF la kuomba kuwa mwenyeji wa michuano ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17.
Malinzi alisema maandalizi ya michuano hiyo yatachukua muda wa miaka mitano, ikiwa ni mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

0 comments:
Post a Comment