zanzibar

AZAM WAANZA VYEMA, ASHANTI WAKICHEZEA KICHAPO

Mabingwa watetezi wa kombe la mapinduzi Azam FC wameanza vyema safari ya kuitetea ubingwa wa kombe hilo baada ya kuwachapa Spice star goli 2-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amaan.

Hadi dakika 45 zinakamilika, si Azam wala Spice aliyekuwa ameliona lango la mwenzake.

Azam ilijipatia bao lake la kwanza dakika ya 63, likifungwa na Brian Omony kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Spice, Mohamed Silime, kabla ya Himid Mao kupachika la pili dakika ya 70.

Licha ya Spice kucharuka wakitaka kupata walau bao la kufutia machozi, vijana wa Azam nao walikuwa imara kuokoa hatari zote, hivyo Azam kuvuna pointi tatu.

Katika Uwanja wa Gombani Pemba, Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), na Chuoni ya Zanzibar zilitoshana nguvu ya mabao 2-2.

 

Pia Ashanyi united imeanza vibaya michuano hiyo baada ya kubali kufungwa goli 1-0 na tusker ya Kenya katika mchezo wa pili uliochezwa katika uwanja wa Amani.

Bao pelee la ushindi la Tusker lilitiwa kimiani katika dakika ya 24 kupitia kwa Joshua Oyoo akiunga krosi ya Ali Abondo.

Kikosi cha Azam FC jana: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Bolou, Himid Mao, Salum Abubakar, Mamadou Kone, Kipre Tchetche na Khamis Mcha.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.