Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic ametua mjini Zanzibar na
kujiunga na kikosi cha Simba kinachoshiriki michuano ya Kombe la
Mapinduzi.
Simba ilianza michuano hiyo ikiwa chini ya Kocha Selemani Matola
aliyekaimu nafasi ya Logarusic aliyekuwa kwao nchini Croatia kwa
mapumziko.
Logarusic alisema ameisharejea na kujiunga na kikosi hicho kwa ajili
ya michuano ya Mapinduzi.
"Niko Zanzibar, nilipumzika kidogo jijini Dar es Salaam kabla ya
kuanza safari ya Zanzibar, niko hapa na nimefurahi kuungana na vijana
wangu tena," alisema.
0 comments:
Post a Comment