simba

SIMBA, KMKM WAAMBULIA MOJA

Mabingwa wa kombe la mapindzi wa mwaka 2011 Simba SC wameshindwa kuwatambia mabingwa wa Uganda KCC baada ya kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kundi B uliochezwa katika uwanja wa Amaan usiku huu.

Kipindi cha pili Simba ilionekana kuimarika zaidi hasa baada ya kuingia kwa Said Ndemla kuchukua nafasi ya Amri Kiemba na pia Betram Mwombeki aliyechukua nafasi ya Amissi Tambwe, ambaye alionekana kukosa ujanja wa kuipenya ngome ya waganda kwa kudhibiwa vilivyo. Kwa ujumla Simba walipiga mikwaju mingi zaidi iliyolenga lango kwani walipata mikwaju 6 wakati KCC walipiga mitatu

KCC wangeweza kuandika goli la kuongoza katika dakika za mwisho kabisa za mchezo kamasi uhodari wa mlinda lango Ivo Mapunda kuuucheza mpira uliokuwa ukielekea langoni na kufanya timu zote mbili zifune alama moja na kufikisha alama nne.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgBf35nyoMzGJ408bCEbmiEBSOpUav1oNAuLHzPeu37ZVE-ERfzJ2fvLVRtGt0cTP6s-_nt8xV_pnfMjfhzjmqCB95T1FfqZ7WkN0iV4KHnHmuLPoHO5MBm6uPlWEUrC8_NTKO10aSrtXs/s1600/12.jpg
Wakati mchezo wa awali kati ya KMKM na AFC Leopards ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na kupelekea timu hizo kuvuna point moja moja kwa kila mmoja.

KCC iko kilelelni mwa kundi B ikiipiku Simba kwa wingi wa magoli ya kufunga wakati AFC na KMKM zinashika nafasi ya tatau na ya nne kwani zote zina alama moja kila moja. Michezo ya mwisho keshokutwa ndiyo itaamua ni tiu ipi iende robo fainali wakati Simba itakapocheza na KMKM na na KCC wakiikabili AFC Leopards

Kesho Jumamosi kuna michezo mine. Kwenye uwanja wa Gombani Pemba watoza ushuru wa Uganda, URA watapepetana na timu mseto ya Pemba (Clove Stars) kuanzia saa 8 mchana na baadaye saa 10 Mbeya Sita watakipiga na timu ya Chuoni.

Wakati hayo yakiwa Pemba, Unguja kwenye uwanja wa Amaan saa 10 jioni Ashanti United wataonyeshana kazi na timu mseto ya unguja (Spice Stars) na sa 2 usiku mabingwa watetezi Azam watawakabili Tusker ya Kenya.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.