simba

SIMBA WAANZA NA USHINDI, MBEYA CITY WAKIBANWA

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcg0Qt6Q4HPXLrnR2FGi_wchKTFdG4Qhuzdsw6mTEVBUpXFew8AhV9LnFExisHmDMRMvzXNrReDci83siTwzbBHIDYN0RfbQQBhN81xrNmlE0l1kfZYOb9lrPgn1ccSqHam1hz8jDy6yo/s1600/11.jpg


Mabingwa wa kombe la <apinduzi mwaka 2011 Simba SC wameyaanza vyema mashindano hayo yanayo fanyika kila mwaka katika kulekea katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. ambapo Simba SC waliichapa goli 1-0 AFC Leopard ya Kenya.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Unguja, goli pekee la Simba SC lilipatikana kupitia kwa Amri Kiema akiunga pasi ya Amisi Tambwe.



Mchezo wa awali uliochezwa katika uwanja huo wa Amani ulishuhudia waganda KCC wakiichapa goli 3-2 wenyeji KMKM.

KMKM ilikuwa ya kwanza kuandika goli kupitia kwa Khamis Ali Khamis aliyunganisha vema mpira wa kona katika dakika ya saba ya mchezo. KCC walijibu mapigo kwa kusawazisha dakika nne baadaye kupitia kwa Herman Waswa ambaye baadaye alifunga la tatu katika dakika 82 baada ya Tony Oduor kufunga la pili na KMKM kusawazisha dakika 79 kupitia kwa Maulid Ibrahim Kapenta.

Wakati katika uwanja wa Gombani Pemba Mbeya City wamebanwa mbavu na combine ya Pemba baada ya kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya goli 1-1. Mbeya City walitangulia kufunga kupitia kwa Deus Kaseke dakika ya 13 na Pemba combine wakazisha dakika 23 kupitia kwa Mawanga.
 
Kesho kuna michezo miwili yote uwanja wa Amaan wakati mabingwa watetezi Azam watakapomenyana
na Spice Stars (Unguja combine) kuanzia saa 10 jioni na baadaye Ashati United iliyochukua nafasi ya Yanga kumenyana na Chuoni ya Zanzibar

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.