netball

TEMEKE WATETEA UBINGWA WAO

http://m.habarileo.co.tz/images/chaneta-temeke.jpg


TIMU ya netiboli ya Mkoa wa Temeke imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya Kombe la Taifa , baada ya kuifunga Morogoro magoli 52-38 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Temeke walianza kuliandama lango la Morogoro tangu robo ya kwanza ya mchezo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 15-7, pia Temeke walizidi kung’ara kwenye robo ya pili baada ya kuifunga Morogoro magoli 12 - 8.

Kwenye robo ya tatu Morogoro walizidi kupotea na kujikuta wakifungwa magoli 14- 10 na robo ya nne ya kukamilisha mchezo Morogoro walizinduka na kuifunga Temeke magoli 17-14.

Morogoro hawatamsahau mfungaji wa Temeke Mwanaidi Hassan kwani ndiye alikuwa mwiba mchungu kwa kutumbukiza mabao mengi katika mchezo wao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alisema kuwa Temeke wanafanya vizuri na wametetea ubingwa wake kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Anna Kibira aliwapongeza wafadhili waliojitoa kukisaidia Chama chake na kuomba wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu ya Taifa “Kilimanjaro Queens” inayokwenda kwenye mashindano ya Mapinduzi.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.