Wikend

LYON WAICHAPA RUVU SHOOTING

TIMU inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya African Lyon imeinyuka Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Sigara, Dar es Salaam.

Bao hilo lilifungwa na mchezaji mpya, Sadiki Mwimbo aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka timu ya Daraja la Kwanza DRC, Viruga.

Akizungumza na gazeti hili, Kocha wa Lyon, Charles Otieno alisema timu mechi hiyo ilikuwa ni muhimu kwao katika kuangalia upungufu ambao wataurekebisha kama sehemu ya maandalizi ya Ligi Daraja la Kwanza msimu huu.

“Mechi hii imeonesha wazi kuwa tuko vizuri, lakini bado tunaendelea kuangalia kwa sababu lengo letu ni kujenga kikosi kizuri kitakachotuwezesha kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu kwa mara nyingine,” alisema.

African Lyon ilishuka daraja msimu wa 2012/2013, hivyo wamejipanga kurudisha hadhi yao kwa kusajili wachezaji wengi vijana na wakongwe kutimiza malengo yao.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.