MICHUANO ya netiboli Ligi daraja la pili iliyoanza juzi mkoani Tanga inaendelea vizuri ambapo baadhi ya timu zimeanza vyema kuonesha makali yake katika kuhakikisha zinapanda daraja.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Anna Kibira, katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja wa Polisi Chumbageni timu ya Sedico ilianza vyema baada ya kuitandika Peacehill kwa 44-20.
Aidha Jiji Tanga ilianza vibaya mashindano baada ya kukubali kichapo kutoka kwa timu ya Kongowe kwa magoli 20-22. Kwa upande wa Magereza ilianza mchezo huo kwa kasi kubwa baada ya kuwafunga Korogwe mabao 40-0.
Katika mchezo wa pili uliwakutanisha Sedico na Korogwe waliofunga mabao 26-20 na wakati huo, Jiji wakiwafunga Peacehill 43-14. Mchezo wa jana ulizikutanisha timu za Precious dhidi ya Lindi, ambapo Lindi iliondoka na ushindi wa mabao 33-18.
Kongowe baada ya kufanya vizuri katika mchezo wake wa kwanza, ikatengeneza njia nyingine ya mafanikio kwa kuwafunga mabao Peacehill mabao 34-19.
Kwa upande wa Jiji Tanga ambayo ilianza mchezo wa kwanza kwa kufungwa, wa pili ikashinda na wa tatu pia ilifanya vizuri baada ya kuwachakaza ndugu zao Korogwe kwa mabao 29-12.
CHANZO: HABARI LEO

0 comments:
Post a Comment