mtazamo

Wachezaji 11 wanao nifanya niwa nahamu ya Ligi kuu kuanza

Dirisha la usajili likitarajwi kufungwa leo saa sita usiku na ikiwa imebakia siku 10 mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Tanzania Bara upigwa baina ya Azam FC na Simba SC, kisha ligi hiyo kuanza kurindima baada ya wiki moja toka mchezo huo wa ngao ya jamii uchezwe hawa ndio wachezaji ambao wana nifanya nitamani msimu mpya uwanze ili nipate kushuhudia viwango na ubora wao katika msimu wa 2012/13 utakao anza september mosi mwaka huu.


SHABAN HASSAN KADO (MTIBWA SUGAR)

Kado karejea Mtibwa sugar kwa mkopo akitokea kwa mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kwishindwa kuonyesha makali yake aliyo pelekea Watanzania kumtazama kama mbadala wa Juma Kaseja katika milingoti ya timu ya Taifa.

Baada ya kuwa na msimu mzuri akiwa na Mtibwa Sugar katika msimu wa 2010/11 na kuonyesha kiwango kikubwa katika kikosi cha timu ya Taifa, kulipelekea vilabu vya Azam FC, Simba na Yanga kuhusishwa na kuwania saini yake na mwisho wa siku alituwa Yanga na kushindwa kuonyesha cheche zake na kupelekea kupoteza namba katika timu ya Taifa, na Yanga kufikia uwamuzi wa kumrejesha Mtibwa Sugar kuziba pengo la kipa mpya wa Azam FC Deo Munish 'Dida'.

Je Kado ataweza kurejesha makali yake na kupelekea wachezaji wadogo wa mitaani kuendelea kujipachika jina lake, ama zama za Kado zimekwisha ndani ya mda mfupi. Ligi kuu Tanzania Bara itatoa jawabu.


SAMIH HAJI NUHU (AZAM FC)

Baada ya kukosekana kwa takribani msimu mzima baada ya kupata jeraha mwshoni mwa msimu wa 2010/11, alirejea katika kikosi cha Azam FC katika michuano ya Kagame Cup, akitokea benchi katika mchezo wa nusu fainali kati ya timu yake iliyo mlea dhidi ya Vita SC ya DR Congo, ambapo kuingi kwake kulipelekea Azam FC kupata goli la kusawazisha na la ushindi yaliyo tiwa kimiani na Mrisho Ngassa na John Bocco.

Kwa mashabiki na wafuatiliaji wa Azam FC jina hili si geni kwao, kwani kabla ya kuumia alijihakikishia namba ya ulinzi upande wa kushoto, ambao katika msimu wa 2011/12 aliongezwa Waziri Salum aliyeweza kuficha pengo la beki huyo.

Hivi karibuni Waziri amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya hapa na pale na kuwalazimu kocha kumpeleka upand wa kushoto kiraka Erasto Nyoni na kufunguwa mlango kwa Mkenya IbrahimShikanda kuanza.

Je Nuhu atarejesha namba yake na kumuweka benchi Waziri Salum pale Waziri atakapo kuwa nnje ya majeraha, ama ndio utakuwa mwendelezo wa kutokea kwenye benchi hata pale Waziri atakapo kosekana uwanjani na kupeleka Nyoni kutumika upande huo wa kushoto, ligi itatoa jawabu.


JOSEPH OWINO (AZAM FC)

Beki wakimataifa toka Uganda aliyepata kuitendea haki jezi ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC kabla ya kuumia na kusajiliwa na Azam FC, Joseph Owino amerejea tena uwanja akiwa na changamoto ya kupoka namba ya mmoja wapo kati ya Nahodha wa Azam FC Aggrey Morrice na beki anae sifika kwa jihadi Said Moradi.

Owino alirejea uwanjani katika michuano ya Urafiki kwa kucheza sambamba na Agrrey na kuonyesha kiwango kilicho peleka arejeshwe kwenye timu ya Taifa ya Uganda, lakini partner yake na Morrise haikuridhisha aliyekuwa kocha wa Azam FC Stewart Hall, hivyo katika hatua ya robo fainali katika michuano ya Kagame alimrejesha bench beki huyo anaesifika kuchezesha timu, na kumrejesha Said Morrad kikosini na kuipeleka Azam FC fainali ya michuano hiyo.

Morad na Aggrey walikuwa na msimu mzuri katika msimu uliomalizika kwa Azam kushika nafasi ya pili huku ikimaliza ikiwa imeruhusu magoli machache katika nyavu zake kulinganisha na msimu ujao.

Je Owino atafanikiwa kupenya ama kitamkuta kilicho mkuta beki toka Ghana aliyesajiliwa msimu uliopita na Azam FC na kuingia katika orodha ya wachezaji wa kigeni walioshindwa kuonyesha cheche zao na vilabu vya kitanzania.


MBUYU TWITTE (YANGA SC)

 
Beki aliye tamba na APR katika michuano ya Kagame Cup na kuingia katika orodha ya wachezaji ambao usajili wao umekuwa gumzo katika vyombo vya habari nchini Twitte Mbuyu, kwa kitendo cha kuwania na timu mbili kongwe Simba na Yanga na mwishowe mwenye kisu kikali akafanikiwa kumsajili.

Kuna wachezaji wengi waliotawala vyombo vya habari katika usajili wao hapa nchini lakini baada ya msimu wa ligi kuanza walipotea kabisa na kuonekana magalasa na pale walipo rejea mwakao walidhihirisha makali yao vile vile wapo wachache walio weza kudhihirisha ubora wao hapa Tanzania, je Beki huyo kisiki aliyezigombanisha Simba na Yanga atakuwa katika upande gani.

Upanda wa akina Derrick Walulya, Joseph Chikokoti, George Owino, Kabonge, Wahab, Wagaluka na wengineo, ama upande wa Haruna Niyonzima, Joseph Owino, Marehemu Patrick Mafisango, Jerry Santo, Hamisi Kiiza, Emanuel Okwi, Wisdom Ndolovu na Yarw Berko.


JERRY SANTO (COASTAL UNION)

Ni nadra kwa soka la Bongo mchezaji toka nnje ya nchi kuondoka nchini akiwa bado anahitajika klabuni kama alivyo fanya Jerry Santo pale Simba SC, na sasa amerejea tena nchini akiwa katika timu nyingine nayo tumia uzi unao fanana na Simba SC, Coastal Union ya Tanga.

Coastal Union wamefanya usajili ambao kila mdau wa soka wanangoja kuona adhari za usajili huo katika ligi ambayo imezoleka kuwa ligi ya timu mbili.

Santo alikuwepo katika michuano ya kombe la Kagame akiwa na Tusker ya Kenya ambayo ilimaliza bila kuruhusu nyavu zao kuguswa na wao bila kugusa nyavu za maadui. 

Santo husifika kwa pasi zenye macho na kuzuia vyema mashambulizi yasifike langoni mwake kama kiungo mkabaji na wakati mwingine hutumika kama mlinzi wakati.

Je Jerry Santo ni yule yule alikuwa katika mitaa ya Msimbazi ama anakitu cha ziada kitakachoifanya Coastal kurejesha heshima yake nchini.


FRANK DUMAYO (YANGA)

Msimu wa 2011/12 wadau walikuwa wanajiuliza ni namna gani beki Shomari Kapombe atakavyo weza kupenya na kupata nafasi katika kikosi cha Simba SC akiwa ametuka kuiwakilisha vyema timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 pamoja na timu yake ya Polisi Moro kama mlinzi wakati, ambapo Simba  teyari ilikuwa na Nyoso, Yondani, Costa na Walulya.

Lakini mwisho wa siku akapenya na kuwa nguzo imara ya simba SC katika safu ya ulinzi, hivyo hivyo, mashabiki wa Yanga na wadau wa soka la Bongo wanafikilia namna ya chipukizi Franky Dumayo atakavyo weza kuchukuwa namba mbele ya viungo Athuman Iddi Chuji, Nurdin Bakari, Juma Seif Kijiko.

Urejeo wa Athuman Iddi ndio unao waumiza zaidi kichwa wadau kujaribu kumtafutia nafasi chipukizi huyo ambaye teyari ameshajenga partner na kiungo wa Azam FC Salum Abubakary 'Sure Boy' katika kikosi cha timu ya Taifa. Je atapata nafasi katika kikosi cha Yanga na kuwa tegemeo kama alivyo fanya chipukizi Shomari Kapombe.


SHABANI KISIGA (MTIBWA SUGAR)

Jina la shaban Kisiga lilikuwa lishaanza kupotea baada ya Azam FC kuridhika na mchango wake na kumuacha, hivyo kukimbilia Uwarabani, na sasa amerejea na jina lake limeanza kungara katika michuana ya BancABC super 8 kwa kufunga mabao na kutengeneza magol, hivyo kupelekea Mtibwa Sugar kuwa tishio katika michuano hiyo.

Kiungo huyo aliyepata kungara na Bandar ya Mtwara, SC Villa ya Uganda na Simba SC akiwa injini ya magoli katika timu zote alizopitia, hivi sasa ameongeza utaalamu wa kucheka na nyavu na kupeleka kama mdau wa soka la Bongo kungoja walicho nacho chuo ca kuibua na kuwarejesha mchezoni wa Kongwe walicho nacho msimu mpya.


KHAMISI MCHA (AZAM FC) 

Mzanzibar aliyekuwa anapata nafasi chache za kucheza katika kikosi cha Azam na kuonyesha kiwango chema, huenda msimu mpya akapata nafasi zaidi baada ya Mrisho Ngassa kuondolewa kwa mkop, hivyo kufunguwa mwanya kwa chipiukizi huyo kudhihirisha ubora wake.

Mcha mara zote alizo kuwa anapata nafasi amekuwa akizitumia vizuri, na mara zote nilikuwa nina hamu akipata muda wa kutosha wa kucheza na bila shaka msimu ujao ataupata, lakini je ataweza kudhihirisha ubora wake pale atakapo kuwa anacheza mara kwa mara, jawabu ni msimu mpya.


MRISHO KHALFAN NGASSA (SIMBA SC)

Msimu uliopita Simba SC walikuwa tishio zaidi katika upande wa kushoto kutokana na Emmanuel Okwi kupenda kutokea upande huo katika kushambulia, kuongezwa kwa Ngassa katika klabu ya Simba SC kuna maanisha Simba sasa watakuwa tishio pande zote mbili kutokana kufanana kwa Ngassa na Okwi katika kuziona nyavu, kupunguza wachezaji hata kasi.

Kivutio kikubwa kinacho ngojwa ni pale Simba watakapo kutana na Yanga na sawli pekee linalo ngoja na kuwaumiza kichwa je Simba watamshutumu Ngassa kama akishindwa kudhihirisha makali yake katika mchezo huo, kwani kilicho mtoa Azam FC ni kitendo cha kubuso nembo ya Yanga, kikitafsiliwa kuonesha mapenzi aliyokuwa nayo kwa Yanga ambapo hakuna kitu kibaya kwa Yanga ama Simba kama kupoteza mchezo unao wakutanisha.


SAID BAHAMUZI (YANGA)

Bahamuzi amekuwa gumzo baada ya kuibuka mfungaji bora katika michuano ya Kagame Cup na kiwango kizuri alico kionesha katika michuano hiyo, ila tatizo la washambuliaji wa Tanzania na wachezaji wa nafasi nyingine ni kudumu katika kiwango chake.

Kitendo hicho kinapelekea kuwa na hamu ya kushuhudia mbio za ufungaji bora katika msimu ujao kama jina la Bahamuzi litaendelea kuwemo mpaka mwisho mwa msimu, kwani umekuwa marahdi kwa wachezaji wetu kuwa na viwango vya kupanda na kushuka.

Akiwa Mtibwa Sugar alifanikiwa kuifungia Mtibwa Sugar magoli muhimu na katika msimu uliokwisha ndie mchezaji aliye ifungia magoli mengi Mtibwa Sugar akifuatiwa na Hussein Javu.


JERRY TEGETE (YANGA SC)

Mshambuliaji aliye aminiwa na Marcio Maximo kuwa hazina ya Tanzania, lakini ameshindwa kudhihirisha ubora wake mara baada ya kocha huyo kutoka Brazil  kuondoka nchini huku Swahiba wake Mrisho Ngassa kuondoka Yanga.

Msimu mpya ameletewa changamoto mpya ya kusaka nafasi mbele ya Bahamuzi na Kiiza huku kwenye benchi Chipukizi anae zijua nyavu zilivyo Msuva aliyesajiliwa toka Moro united akimtishia hata kukaa kwenye benchi la Yanga.

Huu msimu unaweza ukawa wa mwisho kwa jina la Tegete katika soka la Bongo kama hato kuwa makini na kusaka namba kwa udi na uvumba akianzia pale pale alipopatia ujiko wa kutokea benchi na kubadili matokeo 'Super Sub'. Ila kama ataendelea na kiwango alicho kionyesha katika michuano ya Kagame huenda tukaona mwisho wa Tegete ndani ya Yanga.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.