Mashindano hayo yatakayomalizika rasmi Januari 13, mwaka huu yameshirikisha timu kutoka Dodoma, Tabora, Arusha, Ilala, Kinondoni, Temeke, Pwani na Mjini Magharibi huku nyingine zikishindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali.
“Mikoa iliyofika imeonesha ari kubwa ya mchezo huu, mimi nawaahidi kuwa timu itakayofanya vizuri itapata zawadi,” alisema.
Alisema kuna haja kubwa kwa Kampuni na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuchukulia mchezo huo kama mpira wa miguu na kuungwa mkono.
Bhanji pia, aliahidi kushirikiana na Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) katika kushirikisha wadau wa michezo umuhimu wa mchezo huo kwa ajili ya kuwavutia kuupenda na kuusaidia.
Alisema ili mchezo huo uwe mzuri kuanzishwe programu maalumu za Shule za Msingi ambazo watoto watakuwa wakielimishwa umuhimu wa mchezo huo, na hatimaye wakue huku wakiwa wanaupenda.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chaneta Anna Kibira alisema ukosefu wa fedha wanaokabiliwa nao na ushirikiano kutokana na vyama vya mikoani ndio ambao umesababisha ushiriki wa timu za mikoani kuwa chache.
CHANZO: HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment