Wikend

4 ZAFUNGANA, WAGOMEA KUINGIA VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO

tmk-788181
TIMU YA TEMEKE MARA BAADA YA KUTWA WAZWA MABINGA WA KOMBE LA TAIFA KWA SOKA LA WANAWAKE

Ligi kuu ya vodacom iliendelea mwishoni mwa juma lililo pita huku kukishuhudiwa fainali ya kombe  la Taifa kwa soka la wanawake na kukiwepo kwa mchezo mmoja wa ligi daraja la kwanza.

Kuna matukio mengi ya,ejiri katika michezo hiyo, ambnapo hapa tutakujuza baadhi ya matukio yaliyojiri ndani na nje ya uwanja yaliyonaswa na dawati letu la Sports In Bongo.

Kwanza kbla ya kuanza na mpenda wadau wa kipengele hiki mtuwie radhi kwa kushindwa kuwepo wiki jana kutokana na msimamizi wa kipengele hiki kuwa katika mitihani.

MATUKIO KATIKA NAMBA

2. IDADI YA MICHEZO AMBAYO HAIKUSHUHUDIA GOLI

Katika michezo sita ya ligi kuu ya vodacom ni michezo miwli tu ambayo imemalizika bila kushuhdia goli lolote lile.

Michezo hiyo ni Yanga na Ndanda FC uliochezwa katika uwanja wa Taifa na ule kati ya Coastal Union na Mtibwa sugar.

Nnje ya Mtibwa sugar, yanga, ndandana coastal timu nyingine ambayo haikuona nyavu za wapinzani wao ni Mbeya city pale walipokubali kufungwa goli 1-0 na Polisi Morogoro.

4. IDADI YA TIMU ZILIZO NA POINTI 18

Timu nne zimefikiha idadi ya pointi 18 wakiwa katika nafasi ya tatu mpaka ya sita katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

Timu hizo nne ni pamoja na Mtibwa Sugar, JKT Ruvu, Ruvu shooting na Polisi Morogoro.

Kabla ya michezo ya mwisho wa juma hili kulikuwa na timu mbili pekee zenye pointi 18 ambazo ni Yanga ambayo sasa inapoint 19 na JKT Rvuvu iliyobakia na pointi hizo 18 na hivyo ni timu tatu kati ya nne zilizofanikiwa kufikisha point 18 katika mwishoni mwa juma lililopita.

11. TOFAUTI YA POINTI TOKA ANAEONGOZA LIGI NA TIMU YA MWISHO

Wakati timu 6 kati ya 14 ziki kamilsha michezp ya mzunguko wa kwanza mwishoni mwa juma lililopita tofauti ya pointi kati anae ongoza ligi Azam FC na aliyemwisho Prisons ni pointi 11, ambazo zinadhihirisha namna ligi ya msimu huu ilivyo kuwa na matokeo ya kustaajabisha.

Ni nadra kukuta mpaka kuelekea mwisho wa mzunguko wa kwanza timu ya mwisho bado ina nafasi ya kushika nafasi mbili za juu za ligi.

Kati ya Azam FC na Kagera Sugar inayoshika na fasi ya 10 kunatofauti ya pointi 6 ambazo kimahesabu zinawezakupunguzwa, hivyo timu zote 10 bado zipo kwenye mbo za kusaka ubingwa msimu huu.

90. WACHEZAJI WA WILI WANYIMWA KADI KATIKA DAKIKA YA 90

Katika mchezo kati ya Yanga na Ndanda, beki wa Ndanda FC alizawadiwa kadi nyekundu katika dakia ya 90 za mchezo, vile vile katika mchzo kati ya Ruvu shooting na Stand United, mchezaji wa Stand United alipewa kadi ya nyekundu katika dakia ya 90.

Kutolewa kwa kadi hizo nyekundu kulielekea timu hizo kumaliza dakika za nyongeza wakiwa pungufu, na huenda kadi hizo zikawa na adahari katika mchezo ambao utawakutanisha Stand United na Ndanda FC mwishoni mwa juma katika uwanja wa Nagwanda sijaona.

MATUKIO NNJE YA NAMBA

TIMU ZAGOMEA VYUMBA VYA KUBADLISHIA NGUO

Katika mchezo kati ya Coastal union na Mtibwa sugar hakuna timu ya iliyoingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya uwanja wa Mkwakwani wakati wa mapumziko.

Wakati wa mapumziko kila timu ilijikusanya pembeni na kupeana mawaidha kabla ya kurejea kwa kipindi cha mpiri ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya billa kufungana.

Kwa mujibu wa tetesi zilizotufikia zinasema kuwa timu hizo zilikataa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa hofu ya ushirikina.

KIONGOZI SIMBA SC ADAIWA KUPULIZIA DAWA

Kiongozi mmoja wa Simba SC alizuiwa asiingie katia vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wakati wa mapumziko akidaiwa kuwa ana desturi ya kupulizia dawa katika chumba wanacho kitumia simba sc kubadilishi nguo .

Dawa hiyo inayodaiwa anaipulizia ina daiwa kuwachosha wachezaji pale wanaporejea katika kipindi cha pili na kupelekea Simba SC kufanya vibaya katika kipindi cha pili.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa Simba SC dhidi ya JKT Ruvu uliomalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

USHINDI KULINGANA NA NAFASI

Katika kombe la taifa kwa soka la wanawake, ambapo fainali yake ilifanyika jana, kulishuhudia timu ikishinda idadi ya magoli ya nafasi iliyo twaa.

Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Ilala waliiifunga Kigoma goli 3, na katika mchezo wa fainali ambao ulishuhudia Temeke akiwa bingwa wa kwanza wa michuano hiyo. Temek waliifunga Pwani goli 1.

ZAWADI YA JUMA: SSERUNKUMA AKISHINDA KILIO KWA YANGA

Baada ya Danny Sserunkuma kufunga katika michezo miwil ambayo ilifuatiwa na sare kqwa upande wa yanga unaweza sema kila akifunga goli, mchezo wa yanga katika mwisho wa juma hilo unamalizika kwa sare ya bila kufungana.

1. Januari 17, Sserunkuma alishinda goli 1 katika ushindi wa wa goli 2-0 wa Simba SC, siku hiyo hiyo Yanga wakatoka sare ya bila kufungana na Ruvu shooting.

2. Januari 31, Sserunkuma alifunga magoli mawili katika ushindi wa wa goli2-1 wa Simba SC, yanga wakatoa sare ya bila kufungana februari mosi.

MATOKEO YA MWISHONI MWA JUMA LILILOPITA

LIGI KUU YA VODACOM

T.PRISONS 1-1 KAGERA SUGAR
POLISI MORO 1-0 MBEYA CITY
SIMBA SC 2-1 JKT RUVU
YANGA 0-0 NDANDA FC
RUVU SHOOTING 2-1 STAND UNITED
COASTAL UNIO 0-0 MTIBWA SUGAR

KOMBE LA TAIFA KWA WANAWAKE

TEMEKE 1-0 PWANI
ILALA 3-0 KIGOMA

MASHINDANO YA TP MAZEMBE

AZAM FC 2-2 ZESCO UNITED
TP MAZEMBE 3-1 DON BOSCO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.