netball

CHANETA KUKUTANA APRILI 5


http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Ana%20Bayi(7).jpg

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Aprili 5, imeelezwa.

Mwenyekiti wa Chaneta, Anna Kibira alisema jana kuwa mkutano huo ambao utakuwa na ajenda mbalimbali, utafanyika ama Dar es Salaam au Arusha. Alisema hawajaamua rasmi wapi mkutano huo ufanyike kwani itategemea na fedha watakazopata.

Kibira aliwataka wajumbe wote wa mkutano huo mkuu kujiandaa kwa ajili ya kushiriki katika mkutano huo mkuu wa kawaida wa kila mwaka.

Aliwataja wajumbe wanaoruhusiwa kushiriki mkutano huo ni pamoja na wenyeviti, makatibu na mjumbe mmoja kutoka mikoa yote pamoja na asasi za kitaifa na wawakilishi wawili wa wachezaji.

Alisema kuwa bado wanasaka fedha kwa ajili ya mkutano huo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya netiboli nchini.

chanzo: habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.