netball

NIC, JKT BWENI KIVUMBI NUSU FAINALI

TIMU nne za netiboli za wanawake zimetinga nusu fainali wakati timu mbili za wanaume zimefuzu kwa fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki inayoendelea katika Viwanja vya Gymkhana mjini Unguja, visiwani Zanzibar.

Kwa wanawake, timu zilizofuzu nusu fainali ni bingwa mtetezi Bima (NIC) ya Uganda na Prisons pia ya Uganda kutoka kwa Kundi A na MOICT ya Kenya na JKT Mbweni ya Tanzania Bara.

Mechi hizo za nusu fainali zitachezwa leo kwa bingwa mtetezi NIC kuikabili JKT Mbweni wakati Prisons ya Uganda itacheza na MOICT.

Kwa wanaume ambao walikuwa wakicheza kwa mtindo wa ligi, timu zilizofuzu fainali ni Polisi na JKU ambazo zitacheza fainali saa tisa alasiri kesho kabla ya wanawake kucheza fainali saa 10:30 jioni.

Timu za wanawake zilikuwa 11 ambazo zilipangwa katika makundi mawili ambapo Kundi A lilikuwa na timu sita za NIC, Prisons, JKU, Zimamoto, Uhamiaji na JKT Ruvu, wakati Kundi B lilikuwa na timu tano za JKT Mbweni, MOICT, KCCA, Mafunzo na KVZ.

Kwa mujibu wa msimamo, NIC ina pointi 10, Prisons pointi nane kwa Kundi A na Kundi B, MOICT iliongoza kwa kuwa na pointi nane na JKT Mbweni ilimaliza na pointi sita.


CHANZO: HABARI LEO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.