yanga

TEGETE, SHARMAH KUTO SAFIRI NA YANGA


WASHAMBULIAJI Kpah Sherman, Jerryson Tegete na kiungo Andrey Coutinho, wataukosa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na FC Platinum ya Zimbabwe, kutokana na majeruhi ambayo yanawakabili.

Daktari wa Yanga, Juma Sufian alisema ukiondoa wachezaji hao, wengine waliobaki wote wapo katika hali nzuri kwa ajili ya pambano hilo ambalo limepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii Uwanja wa Mandava nje kidogo ya Bulawayo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Sufian alisema Sherman na Tegete walioumia kwenye mazoezi siku za karibuni wanaendelea na kupata matibabu wakati Coutinho hajawa fiti kutokana na kuanza mazoezi juzi Jumatatu baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

“Wachezaji hao watatu hawatakuwepo kwenye idadi ya wachezaji wanaoelekea Zimbabwe kesho (leo) kutokana na kuendelea na matibabu, lakini wengine wote waliobaki wapo katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo huo,” alisema.

Katika hatua nyingine, mashabiki wapatao 30 wameondoka nchini jana mchana kwa usafiri wa basi kwenda Zimbabwe kuishangilia timu hiyo itakapokuwa inacheza na FC Platinum katika mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro alisema msafara huo unaratajia kuongezeka kwa kuchukua mashabiki 20 jijini Mbeya na Zambia na pia wanatarajia kufungua tawi la Yanga nchini Zambia kabla ya kuendelea na safari ya Harare.

Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa awali, inahitaji sare au ushindi wa idadi yoyote ya mabao ili kutinga raundi ya pili ambayo huenda ikakutana na Benfica FC ya Angola au Etoile du Sahel ya Tunisia.

 Chanzo: habarileo.co.tz

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.