wachezaji

Himid Mao akana


Toka Kwa Millardayo

Mchezaji HIMID MAO wa club ya soka ya AZAM amekanusha stori ambazo zilidaiwa kutolewa na yeye mwenyewe kuhusu nafasi anayoipata kucheza kwenye mechi za AZAM.

Mao amekanusha stori kwamba amekua akilalamika kuhusu kupewa nafasi ndogo, yani muda mfupi wa kuingia uwanjani pale ambapo Azam inacheza.

Amesema sio kweli, japo huwa inatokea wakati mwingine anapata nafasi chache za kucheza, kwa sababu timu yake ni nzuri kwa hiyo wachezaji ni wengi wakali, hivyo kugombania namba ni kitu cha kawaida.

Amesema “sijawahi kulalamika kuhusu kukosa nafasi, zaidi ikitokea hivyo huwa naongeza juhudi, lakini pia nimeshacheza dakika 90 mara nyingi tu”

Himid Mao aliwahi kuwa CAPTAIN wa timu ya taifa ya vijana kwa zaidi ya miaka mitatu.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.