ngumi

MPINZANI WA CHEKA KUWASILI LEO

BONDIA wa Thailand, Kitschai Singwacha anatarajiwa kutua leo Dar es Salaam kupambana na Cheka katika pambano lisilo la ubingwa litakalofanyika keshokutwa kwenye ukumbi wa Sabasaba.

Katibu Mkuu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Antony Rutta alisema jana kuwa bondia huyo atatua leo mchana, na kesho kupima uzito tayari kwa mpambano huo wa raundi 12.

Alisema tayari Francis Cheka ameshafika Dar es Salaam akitokea Morogoro, akiwa ameshafanya maandalizi ya kutosha.

“Cheka ameshafika leo (jana) akiwa tayari ameshafanya maandalizi kwa asilimia 99, kwa hiyo ataendelea kujifua hapa Dar es Salaam hadi Jumamosi ambapo ndio siku yenyewe,”alisema.

Pambano hilo litakuwa la kwanza tangu Cheka atoke jela hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wake kushuhudia kujipanga upya kwa bondia huyo wa Morogoro.

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni siku hiyo ni Kasim Ouma kutoka Marekani ambaye atapigana na Mtanzania, Shaban Kaoneka, huku Mtanzania mwingine, Cosmas Cheka akidundana na Mkenya, Fred Nyake.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.