ngumi

UKATA KUTOZUIA KLABU BINGWA TAIFA KESHO KUANZA

MASHINDANO ya klabu bingwa ya taifa ya ndondi yatafanyika kama yalivyopangwa mjini Kigoma kuanzia Juni 10 hadi 16 licha ya ukata mkali uliopo katika Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), imeelezwa.

Tayari mabingwa watetezi wa mashindano hayo timu za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Magereza zimeshawasili mjini Kigoma kwa ajili ya mashindano hayo.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wataenda Kigoma kwa mafungu ambapo wawili wataondoka leo na wengine Alhamisi kwa ajili ya mashindano hayo, ambayo ni mara ya kwanza kufanyika Kigoma.

Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga alisema jana kuwa, karibu gharama kubwa itagharimiwa na wenyeji mkoa wa Kigoma huku BFT ilikuwa inasaka kiasi cha Sh milioni 5 kwa shughuli za kiutawala.

Mashaga alikiri kukabiliwa kwa ukata lakini alisisitiza kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa mafanikio makubwa na kufikia malengo yao ya kuchagua timu imara ya taifa.


chanzo: habari leo
 

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.