netball

JKU AONYESHA UBABE KWA MAFUN ZO

TIMU ya netiboli ya JKU imeendeleza ubabe kwa Mafunzo kwa kuifunga mabao 48-30 katika mchezo wa Ligi ya Kanda ya Unguja uliochezwa juzi kwenye Viwanja vya Gymkhana mjini Unguja.

Timu hizo zote ni za vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), lakini vimekuwa na upinzani wa jadi na kutoa ushindani wa hali ya juu jambo ambalo hutoa hamasa kwa watazamaji wanaofika kuangalia mchezo huo.

Katika mchezo huo uliochezwa kuanzia saa 11 jioni, JKU iliyokuwa ikiwatumia wafungaji wake, Pili Peter aliyefunga mabao 30 na Dawa Haji ambaye alifunga mabao 18, waliwachezesha mchakamchaka wapinzani wao hao kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Mafunzo ambayo mtaa wake upo Kilimani mkabala na Kambi ya Polisi ya Zanzibar, iliwatumia wafungaji wake Kazija Salum aliyefunga mabao 20 na Mainda Rogers ambaye alifunga mabao 10. Mbali na mchezo huo, saa tisa alasiri uwanjani hapo kulifanyika mchezo kati ya Zimamoto na Sogea ambao ulimalizika kwa Zimamoto kushinda mabao 68-25.

Wafungaji wa Zimamoto walikuwa ni Khadija Farahani aliyefunga mabao 48 akisaidiwa na Asha Ibrahim aliyefunga mabao 20, wakati Sogea wafungaji wake ni Rukia Haruna mabao 15 na Safinat Mbarak Said mabao 10.

Chanzo: Habari Leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.