ngumi

MABONDIA WATAMBA KUSHINDA CONGO BRAZZAVILLE

KUNDI la kwanza la timu ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 11 ya Mataifa ya Afrika linaondoka leo kwenda Brazzaville, Congo huku timu ya ngumi ikitamba kufanya vizuri katika michezo hiyo.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, bondia wazamani Benjamin Mwangata alisema kuwa, licha ya kutokaa katika kambi ya kudumu lakini ana matumaini ya kufanya vizuri kutokana na ubora wa mabondia wake.

Alisema aliwaandaa vizuri mabondia wake, ambao ni Said Hofu (fly), Hamad furahisha (feather) na Ismail Isack `Gariatano’ (light).

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya alisema jana kuwa, timu ya ndondi itakuwa ya kwanza kuondoka leo kwa kuwa mabondia wataanza kuchuana Septemba 2. Lihaya alisema kuwa michezo mingine inatazamiwa kuanza Septemba 4 na kuendelea.

Timu hiyo ya ngumi itaondoka leo usiku na ndege ya Ethiopia . Timu ya soka ya Twiga Stars pamoja na ile ya kuogelea zitaondoka Jumanne Septemba mosi huku timu ya palarympic, judo na zenyewe zitaondoka Septemba 11.

Chanzo: Habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.