CECAFA

MAGULI AIONGOZA STARS IKIIIADHIBU SOMALIA


Mshambuliaji wa Stand united Elius Maguli ameendeleza wimbi lake la kufumania nyavu baada ya leo kufunga magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza wa kombe la chalenge iliyoanza jana nchini Ethiopia.

Maguli anaetumikia timu ya Taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro stars) leo amefunga magoli mawili kati ya manne waliyofunga Kilimanjaro stars katika mchezo wa mapema uliochezwa leo.

Kilimanjaro Stars leo walikuwa wanacheza na Somalia ambapo mpaka dakika 90 zina mal;izika Kilimanjaro stars walikuwa mbele kwa goli 4-0.

Alikuwa John Bocco aliyefunguwa ukurasa wa magoli kwa Kilimanjaro stars katika dakika ya11 kabla ya Maguli kuifungia Stars goli la pili katika dakika ya 27 na kuipeleka Kilimanjaro stars mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Katika dakika ya 53 Elius Maguli aliiandikia Stars goli la 3 kabla ya John Bocco kuhitimisha katika dakika ya 56 kwa uifungia Kilimanjaro stars goli la 4.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.