Macho ya mshika kibendera Helda yameiokoa Azam FC kutokupata kichapo mbele ya Mtibwa sugar baada ya kukataliwa goli lao katika dakika ya 87 kwa madai Ramadhan Shiza Kichuya mfungaji wa goli hilo kudaiwa ameotea.
Katika mchezo wa leo wa kombe la mapinduzi uliochezwa katika uwanja wa Amani Mtibwa sugar walitawala kipindi chote cha kwanza na kuifanya Azam FC kucheza mchezo wa kujihami zaidi.
Azam FC katika kipindi cha kwanza wamefanya jaribio moja langoni mwa Mtibwa sugar huku Mtibwa sugar wakifanya majaribio matano langoni mwa Azam FC bila mafanikio.
Kipindi cha pili Azam FC walianza kwa kuwaingiza Franky Domayo na Kipre Tcheche kuchukuwa nafasi ya Ame Ally na Khamisi Mcha Viali, mabadiliko yaliyopelekea mchezo kuwa sawa.
Katika dakika ya 61 makosa ya beki David Mwantika na Sadi Morad yanawazawadia Mtibwa sugar goli kupitia kwa Husein Javu akipokea pasi toka kwa Ramadhan Kichuya ambaye alipokea mpira uliokuwa njiani kumuelekea Mwantika ukitoka kwa Morad.
Kuingia kwa goli hilo kulibadilisha muelekeo wa mchezo, huku Mtibwa sugar wakionekana kupunguza kasi na Azam FC wakicheza kwa nguvu kutafuta goli la kusawazisha.
Kocha Stewart Hall aliwanyanyua John Bocco, Waziri Salum na Jean Mugereneza kuchukuwa nafasi ya Allan Wanga, Gardiel Michael na Himid Mao, huku Mecky Mecxime akimuingiza Henry Joseph kuchukuwa nafasi ya Ibrahim Jeba.
Mabadiliko hayo yaliwazawadia Azam FC goli la kusawazisha kwa mkwanju wa penati uliopigwa na John Bocco baada ya kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.
Kuingia kwa goli hilo lilongeza kasi kwa Mtibwa sugar kusaka goli la kuongoza huku Azam Fc wakikosa utulivu katika eneo la ulinzi lililokuwa linaongozwa Said Moradi hii leo.
Katika dakika ya 87 krosi safi ya Issa Rashid inamkuta Ramadhani Kichuya na kuundumbukiza moira nyavuni lakini mshika kibendera akalikataa goli hilo kitendo kilichopelekea mwamuzi kutoelwa uwanjani chini ya ulinzi wa askari mara baada ya ,mchezo kumalizika.
Kwa matokeo hayo ya sare ya goli 1-1, yanaifanya yanga kuendelea kuongoza kundi B wakiwa na pointi 3 wakifuatia na Azam FC na Mtibwa sugar wakiwa na pointi 1, huku Mafunzo wakiwa wa mwisho bila ya pointi.
0 comments:
Post a Comment