Ligi kuu ya vodacom imemalizika hapo jana na kushuhudia Simba SC wakitwawazwa Mabingwa wapya wa ligi hiyo, huku Azam FC wakipata nafasi ya kuiwakilisha nchi na Polisi Dodoma, Moro united na Villa squad wakishuka daraja.
Kuna matukio mengi yaliyojitokeza msimu huu likiwemo la hart-trick moja, shutuma za upangaji matokeo na yafuatayo ni matukio 10 yaliyonaswa na SIB msimu huu katiki ligi kuu ya Vodacom 'VPL':
10. TIKETI
Tiketi zilizotumika katika michezo ya awali takribani yote haikuwa tiketi za mchezo husika, bali zilikuwa ni tiketi ya michezo ya misimu ya nyuma huku vilabu vikikatwa katika makato ya getini gharama za kuchapisha tiketi.
9. LESENI ZA WACHEZAJI
Mechi za mwanzo wa msimu timu nyingi ziliadhirika baada ya wachezaji wake wapya kucheleweshewa leseni zao nahivyo kushindwa kutumika katika mchezo husika, huku yanga wakifanikiwa kuwatumia.
TFF walichelewa kutuma leseni za wachezaji ambazo zina waruhusu kutumiki klabu husika katika VPL, hivyo wachezaji hao ambao leseni zao zilichelewa kutumwa kwa uzembe wa TFF walishindwa kutumika katika michezo ya kwanza.
8. MBWA WA BOBAN
Katika mchezo uliochezwa hapo september 21 kati ya Simba na Toto Africa, mbwa wa Askari alikata kamba na kuingia uwanjani katika dakika ya 29 na kumfukuza Haruna Moshi Boban, na Felix Sunzu wa Simba, lakini mbwa huyo aliwahi kudhibitiwa kabla ya kuleta madhara.
7. USHIRIKINA
a. JKT Oljoro walihusishwa na imani za kishirikina kufuatia utaratibu walio kuwa nao wakuwa wa mwisho kuingia uwanjani na kuzunguka katika mstari wa mwisho wa eneo la kuchezea mpira mara mbili kisha kukimbia katika mstari wakati wa uwanja na kuweka duara katikati ya uwanja.
Katika mchezo kati ya Oljoro na Azam FC uliochezwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi, wachezaji wa Azam FC walizuia wasikamilishe uwanja kwa kusimama kwenye mstari wa upande waliokuwa wanaufanyia mazoezi.
Mmoja wa watu wa Azam FC waliingiwa na shaka na mwakilishi wa SIB aliyekuwepo uwanjani hapo akidhani ninaweka kitu uwanjani wakati akiwa ndio kwanza amewasili uwanjani, akiwaangalia wachezaji wa Azam FC karibu na uzio wa eneo la uchezaji.
b. Kipa wa Toto Africa alionekana akifukia kitu golini mwake kipind cha pili katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Taifa machi 11 mwaka huu. Kitendo kilipelekea Sunzu kupiga mpira nyavuni mwatoto huku Nyoso na wachezaji wa simba wakijaribu kukitafuta kilicho fichwa pale mpira uliposimama. Mwisho wa mchezo Toto 0-0 Simba.
6. UPINZANI WA JADI
Simba walitishia kugomea ili mchezaji wao Kago apitishwe baada ya usajili wake kuingia dosari. Yanga wao walitaka walipwe mil 16 zao kabla ya mchezo huo wa ngao ya hisani baina ya watani hao wajadi.
Mchezo huo wa Ngao ya jamii, ulichezwa katika uwanja wa Taifa, ambapo Simba SC walitwaa ngao hiyo ya hisani.
5. MAAMUZI YA KAMATI ZA TFF
Kamati za TFF ziligongana katika maamuzi ambazo ni Kamati ya Ligi na Kamati ya Nidhamu na usuluhishi:
a. USHINDI WA MEZANI
Azam FC walipewa ushindi wa mezani baada ya mtibwa sugar kutoka nnje ya uwanja katika dakika za lalasalama matokeo yakiwa 1-1, mchezo huo ulichezwa april 23 katika uwanja wa Azam.
Ushindi huo ulitolewa na kamati ya ligi, lakini kamati ya nidhamu na usuluhishi iliamuru mchezo urudiwe na kuchezwa katika uwanja wa taifa mei 4, ambapo Mtibwa waliifunga Azam 2-1.
b. KUPUNGUZWA KWA ADHABU NA KUBATILISHWA.
Kamati ya Ligi waliwafungia wachezaji wa Yanga kufuatia vurugu baina ya Yanga na Azam lakini kamati ya nidhamu ilibatilisha adhabu hizo na kutoa adhabu mpya iliyo wapunguzia vifungo wacheza hao wa yanga.
4. VIJIMAMBO VYA YANGA
Kuna matukio yaliyofanywa na Yanga msimu huu, ambayo hutarajii kuyasikia yakifanywa na timu kubwa kama yanga:
a. YANGA WAMTUMIA MCHEZEJA MWENYE AZABU
Yanga walimtumia Nadir Haroub Katika mchezo dhidi ya Coastal Union ambapo alitakiwa kuukosa, kutokana na kadi nyekundu aliyoipata kutokana na vurugu katika mchezo dhidi ya Azam.
Canavaro alitakiwa kukosa michezo 3 na badala yake alikuwa teyari amekosa michezo 2, hivyo Yanga kulimwa point 3 walizovuna katika mchezo husika, ambao walishinda goli 1-0.
b. WACHEZAJI YANGA WACHEZA NA BUKTA YENYE NAMBA SAWA.
Omega Seme na Juma Seif Kijiko waliteremka katika uwanja wa Mkwakwani wakiwa na bukta yenye namba 9 katika mchezo dhidi ya Coastal Union, kitendo ambacho Mwamuzi na Kamisaa hawakikuona.
Kijiko jezi yake ya juu ilikuwa ni namba 29 mgongoni ambayo ndiyo anayo ivaaga wakati Seme jezi yake ilikuwa na namba 9 mgongoni
3. VITUKO VYA WAAMUZI
Waamuzi wamekuwa wakilaumiwa kwa maamuzi yao ambayo yalikuwa yanaonyesha kuelemea upande mmoja. Pamoja na hayo kuna vituko walivyo fanya msimuu huu:
a. MCHEZAJI ATOLEWA BILA KADI NYEKUNDU
Katika mpambano wa Villa Squad na Simba uliochezwa Taifa february 4, mchezaji wa Villa Lewis Cosmas alizawadiwa kadi 2 za manjano bila kupewa nyekundu akiwa anatoka nnje kwa matibabu Villa walitaka kufanya mabadiliko kwa kumtoa Lewis lakini Mwamuzi akisaidiwa na mwamuzi msaidizi alikataa na kupelekea Lewis kutoka nnje kwa kadi 2 za manjano bila ya kupewa kadi nyekundu.
b. AMALIZA MCHEZO KABLA YA DAKIKA 90.
Mchezo wa Azam na Mtibwa Sugar uliochezwa april 23 katika uwanja wa Azam ulihitimishwa katika dakika ya 87 na mwamuzi wa mchezo huo na kupelekea kamati ya Nidhamu kuamuru mchezo kurudiwa kwa kuwa makosa alikutwa nao mwamuzi, si timu shiriki katika mchezo huo.
2. LOGO ZA JEZI
Msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom kuliibuka utata wa logo/nembo katika jezi za timu:
a. YANGA KUGOMA KUWEKA DOA JEKUNDU.
Klabu ya yanga waligoma kuweka nembo ya vodacom yenye doa jekundu kwenye jezi zao na badala yake kubadilishiwa nembo na kupewa nyeusi baada ya vuta ni kuvute.
b. AFRICA LYON KUVAA NEMBO YA SEATTLE SOUNDERS.
Klabu ya African lyon walianza ligi wakiwa na jezi yenye logo ya klabu ya Marekani inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo Seattle Sounders, na kupelekea nyezi hizo kuwa na logo mbili za klabu.
Kitendo hiko kilizua utata baina ya TFF na African Lyon.
1.UTATA MICHEZO YA AZAM
Machi 10 wachezaji wa yanga walimvamia mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Azam, baada ya Haruna Niyonzima kupewa kadi nyekundu.
Mwamuzi alipigwa na wachezaji wa Yanga na kupeleka Nadir Haroub kupewa kadi nyekundu. Tukio hilo liliambatana kwa mashabiki wa yanga kukamatwa na askari pamoja na viti vya uwanja wa taifa kuvunjwa.
April 14 mwamuzi wa mchezo kati ya Azam na Polisi Dodoma alipigwa na mashabiki baada ya mchezo kwa kusadikiwa kuibeba Azam katika mchezo huo ulimalizika kwa azam kushinda 1-0.
0 comments:
Post a Comment