FDL

RUVU SHOOTING WAREJEA VPL, FRIENDS, ASHANTI LYON KAZI IPO KUNDI A

Mbio za kusaka nafasi ya kushiriki ligi kuu ya vodacom msimu ujao toka kundi B, umeitimishwa leo na Ruvu Shooting baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa leo.

Ruvu shooting ikiwa imebakisha michezo miwili kukamilisha ligi daraja la kwanza wamefanikiwa kutinga ligi kuu baada ya kufikisha point 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile kutoka kundi hilo.

Ruvu shootinng wakitumia wachezaji wake walio shuka nao daraja chini ya kocha Tom Olaba wamefungwa mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja katika michezo 12 waliyocheza.
Ushindi walioupata leo Friends Rangers wagoli 3-1 mbele ya Ashanti United umeliweka katika wakati mgumu kundi A, ambapo huenda mpaka mchezo wa mwisho ndio unaweza kuamua nani wa kupanda ligi kuu ya vodacom.

Magoli ya Friedns Rangers yamefungwa na Cosmas Lewis aliyefunga magoli mawili huku goli moja jingine likifungwa na Joseph John, huku goli la Ahsnat United likifungwa na Daruweshi Saliboko.

Kwa matokeo hayo ya leo Friends Rangers imefikisha pointi 20 wakiwa nyuma kwa pointi 3 toka kwa vinara African lyon huku Ashant united iliyopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 22 na KMC FC wakiwa na pointi 21.


MATOKEO YA MICHEZO YA LEO

FRIENDS RANGERS 3-1 ASHANTI UNITED
LIPULI 1-2 RUVU SHOOTING
POLISI DAR 0-2 KMC FC
JKT MLALE 1 - 0 NJOMBE MJI

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.