FDL

AFRICAN LYON YAREJEA VPL, YATOA SARE NA ASHANTI


Timu ya kwanza kuifunga Azam FC katika uwanja wa Azam complex African Lyon imefanikiwa kurejea ligi kuu ya Tanzania bara baada ya leo kutoka sare ya goli 1-1 na Ashanti united na kupeleka kufikisha jumlay pointi 27.

African lyon imehitimisha mchezo wake wa mwisho wa ligi daraja la kwanza hii leo, kwa sare hiyo, ambapo mpaka wanaenda mapumziko Ashanti united walikuwa nyuma kwa goli moja.

Ashanti united walisawazisha goli hilo katika kipindi cha pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1 na kuifanya African lyon kurejea ligi kuu ya vodacom.

African lyon katika ligi kuu ya vodacom kabla haijashuka inakumbukwa kwa kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC katika uwanja wake wa Azam complex, huku timu nyingine iliyofanya hivyo ni JKT Ruvu.

Vilevile African lyon wameshawahi kuleta mgonngano kati yao na TFF baada ya kupata udhamini toka kwa Zantel ambao ni washindani wa Vodacom.


MATOKEO YA MMICHEZO MINGINE YA LIGI DARAJA LA KWANZA HII LEO

FRIENDS RANGERS 0-1 KILUVYA STAR
POLISI DAR 0-1 POLISI DODOMA
AFRICAN LYON 1-1 ASHANT UNITED

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.