FDL

BWIRE: TUNAKUJA KUSHINDANA VPL

Baada ya kupata ushindi muhimu dhidi ya Lipuli na kujihakikishia kucheza Ligi Kuu msimu ujao, msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amesema klabu yake imejipanga kuleta ushindani na burudani zaidi katika ligi kuu msimu wa 2016-2017.

“Hatujarudi ligi kuu kupiga blah blah tunakuja kufanya kazi tunakuja kuudhihirishia umma na wadau wa ligi kuu kuwa tumejipanga kuleta ushindani mkubwa lakini pia tunalenga kuleta mapinduzi ya kweli katika soka kwani soka la Tanzania si tu Simba, Yanga na Azam maana Watanzania wengi wanaamini hivyo pia, sasa sisi tunakuja kuleta mageuzi ya Soka” Msemaji huyo mwenye lugha ya kuvutia aliuambia mtandao wa Soka360

Akiongezea kuhusu malengo yao ya msimu ujao na uwiano wa msimu wao wa mwisho wa ligi kuu Tanzania Bara Masau alinena

” kila kitu ni mikakati na mikakati ya timu inaanzia kwa kuwa na wachezaji wazuri, benchi zuri la ufundi, kocha mzuri na viongozi wazuri wenye uelewa wa soka pia hivyo sisi tutajipanga katika hilo na tutalifanyia kazi ipasavyo kuhakikisha timu inabaki ligi kuu na inafikia malengo Tofauti kabisa na Mara ya mwisho tulivyokuwa huko”.

Chanzo: soka360.co.tz

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.