ASFC

GEITA GOLD YAITOA TOTO AFRICANS, YAUNGANA NA SIMBA SC NA YANGA ROBO FAINALI

Kikosi cha Toto African kilicho ikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom

Kikosi cha Selemani Matola Geita Gold imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la TFF linalodhaminiwa na Azam Sports baada ya kuifunga goli 1-0 Toto Afican ya Mwanza.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko wakiwa suluhu (0-0).


Kipindi cha pili Geita Gold walifanikiwa kupata goli lililo ipeleka robo fainali na kuwa timu pekee ambayo haishiriki ligi kuu msimu huu kutinga hatua ya robo fainali.


Geita gold inaungana na Yanga SC, Simba SC, Coastal union, Ndanda FC, Tanzania Prisons na Mwadui FC, huku timu ya nane inatarajiwa kufahamika hapo kesho kati ya mchezo wa Panone FC na Azam FC.


Mchezo kati ya Azam FC Panone FC watakuwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Ushirika mkoani Moshi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.