CAF

YANGA WAIONDOSHA APR, WAINGOJA AL-AHLY AMA LIBOLO


Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wamefanikiwa kutinga hatua ya pili ya kombe la klabu bingwa Afrika baada ya kuwaondosha APR kwa jumla ya goli 3-2, baada ya mchezo wa leo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Yanga SC walikuwa wenyeji wa APR katika mchezo wa klabu bingwa Afrika ulichezwa katika uwanja wa Taifa na APR ambao walifungwa goli 2-1 na yanga katika mchezo wa kwanza waliuwanzana mchezo kwa kasi.

Juhudi zao zilkizaa matunda baada ya kupata goli la mapema na kuwafanya yanga kuwa nyuma kwa goli 1-0.

Yanga SC walisaka goli la kusawazisha kwa udi na katika dakika ya 28 Donald Ngoma alimalizia pasi safi ya Thaban Kamusoko na kuiandikia yanga goli la kusawazisha.

Kipa wa yanga Ally Mustpha Bathez leo aliokoa michumo mingin na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Kwa matokeo hayo ya sare na yale ya 2-1, inaifanya Yanga SC kuiondosha APR kwa jumla ya magoli 3-2, na sasa anangoja mshindi kati ya Al Ahly ya Misri na Recreativo de Libolo ya Angola katika hatua ya 16 Bora.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.