Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro ulingo wa Ngumi wa kisasa ambao wizara ilipewa na Serikali ya China kwa ajili ya maendeleo ya ngumi nchini.Wizara imeamua kuwapa jeshi kwakuwa ni sehemu salama na watakuwa na nidhamu ya kuutunza na pia ulingo huo utaimarisha Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania(BAMMATA). Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni mkurugenzi wa michezo jeshini (wa kwanza kushoto) na Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge(wa kwanza kulia). |
Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Kisasa wa Ngumi kwa Jeshi hilo ili wautumie kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mchezo wa ngumi kwani Serikali imeona ni sehemu salama Zaidi na nidhamu ya kuutunza ipo na hata pale utapoitajika kutumika kwingine uchukuliwe na kurudishwa jeshini hapo kwani jeshi hilo limeleta heshima kubwa ya michezo nchini na kulifanya baraza la michezo ya majeshi (BAMMATA) kuimarika zaidi.
“Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na mchango mkubwa sana katika michezo hapa nchini na limetuletea sifa kubwa sana kwetu na hivyo hatukuwa na shaka tulipoletewa ombi la ulingo huu.Ulingo huu utumike vyema na ulete heshima hapa nchini”Alisema Nape.
Aidha Waziri nape alitoa rai kwa jeshi hilo kurudisha michezo jeshini kwani inajenga uzalendo na kuimarisha umoja,undugu na urafiki.
Waziri huyo pia alikazia kuwa wizara yake itaendelea Kwa upande wake Meja Jenerali Issa Nassor ambaye ni mkuu wa mafunzo na Operesheni Jeshini alimshukuru Waziri Nape na Wizara yake kwa kuwapa ulingo huo na kuwa utawasaidia “Ulingo huo utatumika kwa mabondia wote Tanzania kwani utajenga Umoja na Kufahamiana na kukuza michezo na pia tutashirikisha askari wote kwani michezo ni sehemu ya kazi pia”.
Alisema Aidha alisema kuwa Msaada wa Ulingo huo ni chachu ya mazoezi na itawajengea wana mchezo huo chachu ya ushindi na kuwataka wadau mbalimbali wa michezo kuunga mkono jitihada za Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imetoa ulingo huo kwa jeshi hilo baada ya kupewa msaada na serikali ya watu wa china mwaka jana ikiwa ni jitihada za kuboresha jeshi hilo.
kushirikiana na jeshi hilo katika michezo mbalimbali nchini. sana katika suala la mazoezi na hata mashindano mbalimbali. Meja Jenerali Issa. jeshi hilo kwani wana nia ya wazi ya kuwa kituo cha ubora. michezo nchini.
0 comments:
Post a Comment