ASFC

YANGA WAPEWA WAARABU KOMBE LA TFF, HAKUNA MICHEZO DAR NUSU FAINALI


Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wamepangiwa kukutana na Waarabu wa Tanga Coastal union katika hatua ya nusu fainali ya kombe la TFF ambapo mchezo huo utafanyika april 24 mkoani Tanga.

Droo iliyopangwea hii leo inaonyesha kuwa hakuto kuwa na mechi itakayo chezwa jijini Dar es salaam japokuwa kuna timu mbili toka Dar es salaam katika hatua hiyo ya nusu fainali.

Coastal union watakuwa wenyeji wa Yanga SC katika uwanja wa Mkwakwani wakati Azam FC wakikarabishwa katika uwanja wa Mwadui Complex kuwakabili Mwadui.

Michezo hiyo itapichezwa aprili 24 mwaka huu, japo tarehe hiyo imepingwa na wawakilishi wa Azam FC na yanga walioudhuria zoezi hilo.

Jerri Muro msemaji wa yanga na Kawemba katibu mkuu wa Azam FC wote kwa pamoja walisema kuwa ni ngumu watoke katika michezo ya kimataifa aprili 23 na kuunga safari ya kuelekea katika vituo kwa ajili ya michezo ya nusu fainali.


MECHI ZA NUSU FAINALI

MWADUI FC Vs AZAM FC
COASTAL UNION Vs YANGA SC

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.