Mchangani

WAAMUZI 40 KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA


Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeteua waamuzi 40 watakaochezesha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL) inayoanza leo Mei 23 katika vituo vinne tofauti hapa nchini.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27, imegawanywa katika makundi manne ambako bingwa katika kila kundi atapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 ngazi ya taifa kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza Ligi daraja la Kwanza msimu wa 2017/18.

Timu tano zitapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili ambako mbali ya washindi katika vituo vyote vinne, mshindwa bora katika vituo vya Njombe, Morogoro na Singida nayo itapanda daraja kwa kuangalia vigezo vya wingi wa pointi, wastani wa mabao, mabao kufunga na mabao ya kufungwa. Kituo cha Kagera hakijajumuishwa kwa kuwa kina timu shiriki sita.

Waamuzi walioteuliwa kuchezesha ligi hiyo kwa kituo cha Njombe ni Elasto Msaliwa, Klement Manga, Mashaka Lulambo, Lazaro Mbogoro, Michael Mkongwa, Alex Chitalula, Maulid Makiwa, Michael Kilango, Edina Ndelwa na Haidal Kisingile.

Timu zinazoshiriki ni Mkali Stars ya Ruvuma, Mtwivila (Iringa), Sido FC (Mbeya), Jangwani FC ya Rukwa, Nyundo FC ya Katavi, Mawezi ya Morogoro na Zimamoto ya Ilala, Dar es Salaam.

Kituo cha Morogoro walioteuliwa ni Athuman Lazi, Mohammed Theophil, Seleman Kinugane, Fikiri Yusuph ‘Magari’, Nicolaus Makangara, Mwarabu Mumba, Emmanuel Muga, Herry Shao, Shaban Juma na Makongo Katuma na timu zinazoshiriki ni Stend  FC ya Pwani, Mbuga FC (Mtwara), Namungo FC(Lindi), Muheza United ya Tanga, Stand Misuna FC ya Singida, Makumbusho ya Kinondoni na Sifa Politan SC ya Temeke, Dar es Salaam.

Kituo cha Singida wako Meshack Suda, Abdallah Mwinyimkuu, Sarah Bongi, Lucas Mathias, Amani Mwaipaja, Siyachitema Kawinga, Theophil Tegamaisho, Shaaban Msangi, Aboubakar Irume na Frederick Ndahani na timu shiriki ni Veyula FC (Dodoma), Pepsi SC (Arusha), Kitayosce FC (Kilimanjaro), Stand FC (Tabora), Murusagamba FC (Kagera), Fire Stone (Manyara) na Tomato FC (Njombe).

Kituo cha Kagera walioteuliwa ni Jonesia Rukyaa, Jamada Ahmada, Ringston Rwiza, Grayson Buchard, Grace Wamala, Edgar Lyombo, Yahaya Juma, Adrian Karisa, Getrude Kahawa na Ahmada Simba na timu shiriki ni Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela City (Shinyanga), Ambassador FC (Simiyu), Igwe FC (Mara) na Mashujaa (Kigoma).

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.