wachezaji

JEBA: NAHITAJI KUENDELEA KUCHEZA MTIBWA


KIUNGO Ibrahim Jeba wa Mtibwa Sugar, amesema hana mpango wa kuhamia Simba licha ya miamba hiyo ya zamani kumhitaji.

Jeba amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Mtibwa kiasi cha kuzivutia timu nyingi kubwa ikiwemo Simba, ambayo inahaha kuimarisha kikosi chake.

Akizungumza na gazeti hili, Jeba alisema anajua madhara ya kucheza timu kubwa kama Simba, hivyo angependa kubaki Mtibwa sehemu ambayo anapata nafasi kucheza.

“Nashukuru kwa timu kubwa kuonesha imani ya kunihitaji, lakini bado sijafikiria kuondoka Mtibwa, kwa sababu nafurahia maisha ya hapa na hata maslahi ambayo ndio kitu kikubwa katika mchezo wa soka,” alisema Jeba.

Kiungo huyo alisema hapendi kuzichezea timu kubwa kwa sababu mara nyingi huua vipaji vya wachezaji wazawa baada ya kusajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania.

Alisema mipango yake ni kuisaidia timu hiyo kupata mafanikio ikiwemo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu msimu unaokuja baada ya kushindwa kufanya hivyo msimu uliopita.

Hiyo ni mara ya pili Simba kumhitaji Jeba, mara ya kwanza walimchukua kutoka Azam FC, lakini waliachana naye kwa madai ni mgonjwa lakini baada ya kufanya vizuri akiwa na Mtibwa wamerudi tena na kuhitaji mchango wake.

Chanzo : Habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.