vilabu

MSHAMBULIAJI WA PRISONS ATUA MBEYA CITY

Aliyekuwa mshambuliaji wa kutumainiwa wa kikosi cha Tanzania Prison cha jijini hapa, Mohamed Mkopi amejiunga na Mbeya City fc kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Mara baada ya kusaini kandarasi hiyo, Mkopi, aliyewahi kucheza pia kwenye kikosi cha Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani, mkoani Morogoro  alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujiunga na City timu ambayo alikuwa na ndoto za kuichezea  hata kabla ya kusajiliwa na Prison msimu uliopita.

“Kabla sijasajiliwa na Prison ndoto yangu ilikuwa ni kucheza kwenye timu hii, nashukuru Mungu baada ya msimu mmoja hili limefanikiwa, nitakuwa hapa msimu ujao, lengo langu ni kufanya kazi kwa nguvu  ili niendelee kuwa sehemu ya kikosi hiki kwa muda mrefu zaidi” alisema.

Chanzo: mbeyacityfc.com

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.