simba

MZAMIRU: NIMESAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

KLABU ya Simba SC imekamilisha Usajili wa kiungo mahiri wa Mtibwa Sugar, Mzamiru Yassin kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo kuanzia Msimu wa 2016/2017. 

Mzamiru mwenye uwezo wa kupiga pasi za uhakika na anaungana na viungo wengine kwenda kuisaidia klabu hiyo kuweza kufanya vizuri msimu ujao.

"Ni kweli tulikuwa kwenye mazungumzo na Simba ila kwa sasa kila kitu kipo vizuri, nimesha saini nao mkataba wa miaka miwili kuweza kuitumikia klabu hiyo na kushirikiana vizuri na wachezaji wengine ntakaowakuta," . Amesema Mzamiru.

Simba wameweza kupata saini ya mchezaji huyo ambaye atakuja kuongeza nguvu safu ya kiungo ambapo imeonekana wachezaji wake wengi wanashindwa kusaidiana na safu ya ushambuliaji kwenye kutengeneza nafasi za magoli.

Mzamiru anakuwa ni mchezaji wa tatu kuondoka kwenye kikosi cha Mtibwa na ni pigo ligine hasa baada ya mlinzi wa kati Andrew Vicent 'Dante' kusajiliwa na Yanga sc, huku kukiwa na tetesi za Simba kuwataka Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya ambao wote wanaichezea timu ya Taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars.

Huyu anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Simba baada ya Emmanuel Simwanza kutoka Mwadui na Jamal Simba Mnyate kutoka Mwadui na wakiwa wanafanya usajili kimya kimya.

Chanzo: michuzi blog

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.