vilabu

THEMI FELIX MNYAMA KUTOVAA JEZI YA MBEYA CITY MSIMU UJAO

Themi Felix
Mfumania nyavu wazamani wa Kagera sugar aliyekuwa anacheza Mbeya city misimu miwili iliyopita, msimu ujao hatokuwa na timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika na Mbeya city kutokuwa teyari kumuongezea Mkataba.

Themi wakati akiwa Kagera Sugar alikuwa anazisumbua timu kubwa na misimu yake miwili ya mwisho alikuwa anafunga zaidi ya magoli 7 kila msimu, lakini baada ya kujiunga na Mbeya city akakutana na ukame wa magoli, ambapo katika msimu yake yote miwili ameshindwa kufikisha jumla ya magoli 7 katika msimu hiyo miwili.

Katika orodha iliyotolewa na Mbeya city yawachezaji 7 ambao hawataongezewa mikataba Themi Felix ni miongoni mwao.

Kwamujibu wa taarifa hiyo inayopatikana katika mtandao rasmi wa Mbeya city (mbeyacityfc.com) wahchezaji wengine ambao hawata ongezewa mikataba ni pamoja na mlango Haningtony Kalyesubula, walinzi ni  Yusuph Abdalah Sisalo,Deo Julius,Hamad Kibopile,Yohana Morris, Richard Peter Chundu na mshambualiaji Temmi Felix.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.