vilabu

AZAM FC WASHUSHA MSHAMBULIAJI TOKA IVORY COAST

MSHAMBULIAJI Ibrahima Fofana kutoka nchini Ivory Coast ametua nchini mchana huu kufanya majaribio ya kujiunga na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC.

Fofana (26), ametua akitokea timu ya Union Sportive de Ben Guerdane ya Tunisia aliyokuwa akiichezea msimu uliopita uliomalizika Juni 14 mwaka huu, aliyojiunga nayo akitokea kikosi cha Asec Mimosas ya Ivory Coast alikodumu tokea mwaka 2013-2015.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.