Ndoto ya mshambuliaji wa Klabu Soka ya Azam, Farid Mussa kwenda kukipiga nje ya nchi sasa imetimia.
Hayo yamebainishwa na uongozi wa klabu yake ya Azam ambayo imesema mchezaji huyo anatarajiwa kuondoka muda wowote kuanzia sasa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Hispania.
Aprili, Farid alikwenda nchini humo kufanya majaribio katika timu ya daraja la pili ya Tenerife na kufuzu.
Akizungumza na Mwananchi, msemaji wa timu ya Azam, Jaffar Idd amesema wadau wa soka wapuuze taarifa za mitaani zinazodai kuwa mchezaji huyo hatakwenda Hispania.
“Nani aliyekuambia taarifa hizo, achana nazo ni za mitaani, Farid atakwenda Hispania muda wowote, anachosubiri ni kutumiwa viza,” alisema.
Kwa sasa, Farid ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho waliopo Zanzibar kujifua kwa jili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

0 comments:
Post a Comment