Mchangani

GOMS WAICHAKAZA BUGURUNI GOLI 2, NA KUTINGA ROBO

Wachezaji wa Goms Unitred wakishangilia goli lao la kwanza hii leo dhidi ya Buguruni united
Timu kutoka Gongalomboto Goms united wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Buguruni united katika mchezo wa tano wa hatua ya mtoano wa michuano ya Sports Xtra D.r Mwaja Ndondo cup, inayodhaminiwa na Azam TV, Star times, Mwanaspoti na Forplan Clinic.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Bandari, Goms United waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 19 kwa mkwaju wa penati uliopiga na Thabit Nuru, goli lililo dumu dakika zote 45 za kwanza.

Katika mchezo huo ambao mgeni rasim alikuwa waziri mwenye dhamana na michezo Nape, Goms walirejea kwa kasi, na kujaribu kusaka goli la pili huku Buguruni wakisaka goli la kusawazisha.

Goms Untide waliandika goli la pili kupitia kwa Haji Zege katika dakika ya 70, na kupelekea mchezo kumalizika kwa Goms kuibuka na ushindi wa goli 2-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Pamoja na kupata tiketi ya kutinga hatua ya robo faninali, Goms United wamefanikiwa kuondoka na kitita cha shilingi laki 3, huku Buuruni wakiondoka na kitita cha Tsh laki 2.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.