Mchangani

KAUZU NAO WATINGA FAINALI KWA MATUTA

Kauzu FC imefanikiwa kutinga fainali ya Dr. Mwaka Sports Xtra Ndodndo Cup kwa mara ya pili mfululizo na kuwa timu ya kwanza kutinga hatua hiyo mara mbili.

Kauzu FC wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Misosi FC kwa mikwaju ya penati 7-6 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Kauzu Fc itakutana na Temeke Market katika hatua hiyo na kuwa fainali ya kwanza kukutanisha timu toka wilaya ya Temeke, na itakuwa ni mara ya kwanza wilaya ya Temeke kutoa bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Forplan Clinic, Mwanaspoti na Azam TV, ikiwa imeratibiwa na Sports Xtra ya Clouds FM na Chama Cha soka Dar es salaam DRFA.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.